BINTI ALIYEJIVISHA PETE YA UCHUMBA 'AJIOA' MWENYEWE BAADA YA KUKOSA MUME WA KUMUOA


Georgina Wambui 
Georgina Wambui akiongea na mwandishi wa habari Lyn Ngugi (kulia) wakati akimhoji.

Binti mmoja amewashangaza wengi baada ya kuamua kujioa kupitia harusi iliyofana sana. Amini usiamini, Georgina Wambui, alifanya harusi ya kukata na shoka ambapo amejioa mwenyewe na kuiacha familia yake vinywa wazi.

Dada huyo mwenye umri wa miaka 33 amesema alikuwa na mpenzi siku za awali lakini penzi lao likasambaratika na akaanza kuishi bila ya mume.

Mambo yalizidi kuharibika 2014 baada ya kuhusika katika jali iliyomwacha na majeraha mabaya ambayo hadi leo yamemfanya kuwa mlemavu.

"Baada ya ajali, niliwapoteza marafiki wengi ambao walikuwa karibu na mimi. Jambo hilo lilinibadilisha sana na kunipa nguvu. Niligundua si marafiki wote wa kudumu," alisema katika mahojiano na mwanahabri wetu.


Mnamo Juni 1, 2018 familia yake ilishangaa sana wakati aliposherekea siku ya kuzaliwa kwake kwa kujinunulia pete na kuwaeleza marafiki kuhusu mapango wa kutaka kujioa mwaka uliofuata. 

Ahadi hiyo ilitimia Juni 1, mwaka huu alipofanya harusi. "Niliamua kufanya hivyo ili kutosheleza nafsi yangu na ila si eti siamini kuna penzi. Nashabikia ndoa pia lakini nimefanya nipendalo na wala si kulingana na vile jamii inataka," alisema.


Georgina Wambui wakati wa harusi yake ambapo alijioa mwenyewe. 

Wambui aliongeza kuwa alikuwa na matumaini mengi ya kuolewa lakini hakuna mtu aliyejitokeza kumrushia ndoano. "Unaweza kuwa umeamua kusubiri, lakini utasubiri mtu maisha yako yote? Nilitaka sana nimpate jamaa anioe lakini sasa hakuna aliyejitokeza," aliongeza kusema. 

Licha ya kujioa, dada huyo alisema ana matumaini ya kupata mtoto. "Baada ya kufanya harusi, sasa nipanga kumpata mtoto ... hapo ndipo ninapoelekea," alisema. 

Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527