MAURIZIO SARRI AIBUKIA JUVENTUS


 Aliyekuwa meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amejiunga na Miamba ya Italy  Juventus ambapo amesaini kandarasi ya miaka mitatu.

Timu ya Chelsea imethibitisha kocha wake Sarri kuondoka katika timu hiyo na kutua Juventus.

Juventus, wamemtangaza Sarri kuwa meneja wao mpya, akichukua mikoba ya Massimiliano Allegri, aliyeachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita.

Sarri amedumu kwenye kikosi cha Chelsea kwa miezi 11 huko Stamford Bridge, akiwaongoza kubeba ubingwa wa Europa Ligi na kuwarudisha kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post