WAKALA WA VIPIMO (WMA) WAHAKIKI PAMPU KITUO CHA MAFUTA TOTAL MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM


Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa 
wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akifanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu  katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo  ili kujiridhisha kama upimaji mafuta wa Pampu ni sahihi wakati wateja 
wanapofanya manunuzi, Maadhimisho ya vipimo duniani yanatarajiwa  kufanyika Mei 20, 2019 jijini Dar es salaam.
Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa 
wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akishuhudia wakati mafuta yakijazwa kwenye kipimo maalum cha mafuta wakati maofisa hao walipofanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo, kushoto ni Ally Mohamed Meneja wa kituo cha Total Mlimani City. 
Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa 
wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wakati wakifanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu  katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo  ili kujiridhisha kama upimaji mafuta wa Pampu ni sahihi wakati wateja  wanapofanya manunuzi anayejaza mafuta ni Mbaningo Mselem Afisa Vipimo. 
Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa 
wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akionyesha Stika ya uthibitisho kuwa pampu hizo zimekaguliwa wakati maofisa hao waliofanya ukaguzi kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo. 
Ally Mohamed Meneja wa kituo cha mafuta Total Mlimani City akihojiwa na waandishi wa habari kwenye kituo hicho jijini Dar es salaam leo baada ya wakala wa vipimo kukagua pampu na kujiridhisha kuhusu ubora wake wa vipimo.
Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa  wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akihojiwa na waandishi wa habari wa ITV mara baada ya maofisa hao kufanya ukaguzi katika kituo cha  mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo.kushoto ni Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA).
Kituo cha Mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post