WIZARA YA KILIMO YAUNDA TUME MAALUMU KUSHUGHULIKIA UDHAIFU ULIOPO KATIKA MIRADI YA UMWAGILIAJI


Wizara  ya Kilimo imesema imeona udhaifu mkubwa katika miradi ya umwagiliaji hivyo imeunda timu maalum kulishughulikia hilo.

Hayo yameelezwa leo Mei 20 Bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo,Omari Mgumba wakati ahitimisha mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha 2018-2019.

Mgumba amesema ripoti ya CAG imeonesha kuna udhaifu mkubwa katika miradi ya umwagiliaji nchini hivyo Wizara ya Kilimo imeunda timu maalum kwenda kuthibitisha hayo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527