Zaidi ya sh 800 milioni zinatarajiwa kutumika katika zoezi la kuwafunga mikanda ya mawasiliano ya kijiographia(GPS) Tembo ambao wanapatikana hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Makao na Pori la Akiba la Maswa.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangallah jana amezindua mpango huo katika eneo la Makao WMA ambalo imewekeza kampuni ya Mwiba Holding moja ya kampuni zilizochini ya Taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF)
Waziri Kigwangala alisemaVifaa hivyo il vya GPS vitawezesha Tembo kufatiliwa mienendo yao na kudhibitiwa matukio ya Tembo kuvamia mashamba na masuala ya ujangili.
Alisema katika mpango huo pia kutakuwa na uzio wa technolojia ya kielekronik ambao utawezesha kuonekana Tembo ambao wanatoka maeneo ya hifadhi kabla ya kufanya madhara.
Waziri Dk Kigwangallah alipongeza taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) kwa kufadhili mradi huo na kueleza wizara yake ilifanya utafiti na kubaini taasisi hiyo ni miongoni mwa taasisi safi zinazoendekeza uhifadhi.
Waziri Kigwangallah pia alipongeza watafiti kutoka taasisi ya utafiti wa wanyamapori(TAWIRI) kwa kuendesha zoezi hilo.
Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund(FCF) Nicholas Negri alisema mradi huo utasaidia sana uhifadhi nchini na kuvutia watalii zaidi.
Alisema FCF itaendelea kishirikiana na serikali katika kuendeleza uhifadhi kwani pia tayari wamefadhili mradi wa kuwafunga vifaa vya mawasiliano Faru ili kuwalinda na ujangili.
Mtafiti Mkuu wa TAWIRI, Dk Edward Kohi amesema mradi huo,unatarajia kugharimu dola 300,000 ambazo ni zaidi ya sh 800 milioni.
Amesema katika eneo la hifadhi ya jamii ya makao na pori la akiba la Maswa Tembo 18 watafungwa vifaa vya GPS na katika maeneo mengine tayari Tembo 95 wamefungwa GPS.
Mtafiti wa Tawiri Dk Emmanuel Masenga amesema hadi sasa Tembo 95 wamefungwa mikanda ya GPS maeneo mbali mbali ya hifadhi nchini.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo ,Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka alisema mpango huo wa kuwafunga Tembo GPS utasaidia kuondoa migogoro baina ya wa hifadhi na jamii.
Alisema wananchi wamekuwa wakipiga simu mara kadhaa kuomba msaada pale Tembo wanapovamia mashamba yao.
“Sasa Tembo kufungwa GPS ni faraja kwetu lakini pia tunapongeza mwekezaji wetu Mwiba Holdings kwa mradi huo” alisema