URUSI NA UTURUKI KUUNDA MIFUMO YA MAKOMBORA YA S-500

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kuwa nchi yake na Russia kwa pamoja zitaunda mifumo ya makombora ya S-500 baada ya mpango wake wa awali wa kunununua mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Moscow kuzusha mivutano.

Jitihada za Uturuki za kutilia mkazo kununua mfumo wa makombora wa S-400 umezorotesha zaidi uhusiano wa nchi hiyo na Marekani; nchi ambayo imeionya mara kadhaa Ankara kuhusu hatari zinazoikabili vikiwemo vikwazo iwapo itaendelea na mpango wake wa kununua mfumo huo wa makombora kutoka Moscow.

Hata hivyo akizungumza mjini Istanbul, Rais wa Uturuki amesema kuwa na hapa ninamnukuu, "kutakuwepo uundaji wa pamoja wa mfumo wa makombora wa S-500 badala ya ule wa S-400", mwisho wa kunukuu. Ameongeza kuwa makubaliano yamefikiwa, na hapa hakuna swali kwamba Uturuki imeachana na ununuzi wa mfumo wa makombora wa S-400.

Itakumbukwa kuwa, uhusiano kati ya Uturuki na Marekani; nchi mbili ambazo zote ni waitifaki wa Muungano wa Nato umeingia dosari kutokana na masuala kadhaa ikiwemo hatua ya Marekani ya kuwaunga mkono wapiganaji wa Kikurdi wa Syria; wapiganaji ambao Ankara inawataja kuwa magaidi; na pia hatua ya Marekani ya kukataa kumrejesha nchini Uturuki mwanazuoni wa Kiislamu anayetuhumiwa kupanga njama ya mapinduzi dhidi ya Rais Erdogan mwaka 2016.

Wakati huo huo Washington imedai kuwa makubaliano baina ya Ankara na Moscow ya kuunda kwa pamoja mfumo wa makombora wa S-500  ni tishio kwa ulinzi wa Magharibi. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post