SERIKALI YAGAWA BURE KONDOMU KIBAO KWENYE MAENEO YA STAREHE...MAKAHABA WAFURIKA

Maafisa wa afya kaunti ya Narok  nchini Kenya wamesambaza zaidi ya masanduku 4,000 ya mipira ya kondomu huku mamia ya makahaba wakifurika mjini Narok.

 Kulingana na afisa mkurugenzi mkuu wa afya Sereti Mpeti, serikali ya kaunti imegawa kondomu hizo bila malipo katika maeneo ya burudani na kwenye migahawa.

" Hii ni njia moja ya kuzuai kuenezwa kwa magonjwa ya zinaa kwani kaunti hii inatarajia watu mbali mbali kutoka sehemu kadhaa za nchi kufuatia sherehe ya Madaraka ambazo zitafanyika kaunti hii Jumamosi Juni 1," Ms Sereti alisema. 

Sereti pia aliwatahadharisha wakazi dhidi ya kushiriki ngono bila kinga akisisitiza hatari za maambukizi ya magonjwa ya zinaa. 

Imekisiwa kuwa idadi ya wafanya biashara wa ngono itaongezeka kaunti hiyo wakati wa sherehe za Madaraka ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumamosi, Juni 1.

Aidha, kamishna mkuu wa kaunti ya Narok George Natembeya amewahakikishia wakazi usalama wa kutosha wakati wa sherehe hizo. 
Via Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527