SERIKALI YATOA SABABU YA KUVUNJA MKATABA NA KAMPUNI YA KUNUNUA KOROSHO KUTOKA KENYA


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amesema Kampuni ya Indo power ya Kenya iliyokuwa imeingia mkataba wa kununua korosho tani 100,000 ilistahili na ilkuwa halali.

Kakunda ameyasema hayo wakati akihitimisha hotuba yake ya bajeti bungeni jana, Mei 15, ambapo alisisitiza kuwa kampuni hiyo inatambulika nchini Kenya, Afrika Mashariki na dunia nzima.

Alisema kilichosababisha Tanzania kuvunja mkataba huo ni baada ya kampuni hiyo kuchelewa kukamilisha taratibu kadhaa walizokubaliana.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527