Picha : WANAFUNZI WA SHULE YA LITTLE TREASURES WATEMBELEA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN


Wanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga wametembelea kwenye ofisi za Shirika la Save The Children Mjini Shinyanga, kwa ajili ya kupewa elimu namna ya kupinga matukio ya ukatili dhidi ya watoto.


Ziara hiyo imefanyika leo Mei 7,2019 kwa kutembelea ofisi hiyo pamoja na ofisi ya Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga, ili kupewa elimu nanma ya kupinga matukio ya ukatili dhidi ya watoto ili wapate kutimiza ndoto zao.

Akizungumzia ziara hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, Alex Enock, amesema wamefarijika sana kutembelewa na wanafunzi hao wa Little Treasures, ili kuendeleza mapambano ya kupinga matukio ya ukatili dhidi ya watoto mkoani humo.

Amesema watoto wakielewa vizuri masuala ya ukatili itakuwa ni jambo jema, ambapo pale watakapokuwa wakifanyiwa matukio hayo watajua wapi pa kwenda kutoa taarifa ili hatua ziweze kuchukuliwa haraka, na kuweza kuzuia ukatili huo usiendelee kutendeka na hatimaye mtoto kupata haki yake.

“Shirika la Save The Children sasa hivi tunaadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake, ambapo tumekuja na kampeni ya kupinga vita dhidi ya watoto, 'Stop War Against Children', ambayo imelenga kumkomboa mtoto pale vita vinapotokea, ikiwa wengi wamekuwa wakipata madhara kwenye vita hivyo,”amesema Enock.

“Hivyo ziara ya wanafunzi hawa ni faraja kwetu katika kuwapatia elimu hii ya kupinga vita dhidi ya watoto, pamoja na kupaza sauti pale wanapoona mwenzao ama wao wenyewe wanafanyiwa matukio ya ukatili, ili tuweze kupata taarifa mapema na kuweza kuyashughulikia kwa mujibu wa sheria na kuweza kupatikana kwa haki ya mtoto,”ameongeza Enock.

Naye Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale, amewataka wanafunzi hao wakawe mabalozi wazuri kwa wenzao, namna walivyopata elimu hiyo ya kupinga masuala ya ukatili dhidi ya watoto, yakiwamo ya ubakaji, ulawiti, kupigwa, kuolewa ndoa za utotoni pamoja na kuzuiwa kwenda shule.

Nao baadhi ya wanafunzi hao akiwemo Monica Shadraka, wamesema wamefarijika kupata elimu hiyo yakupinga masuala ya ukatili dhidi ya watoto, ambayo itawasaidia kuweza kutimiza malengo yao ya kielimu.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Kaimu mkurugenzi wa Shirika la Save The Children mkoani Shinyinga Alex Enock akiwaelezea wanafunzi kutoka shule ya Msingi Little Treasures namna shirika hilo lilivyoanzishwa hadi kujiingiza kwenye masuala ya kusaidia watoto.

Wanafunzi wa Little Treasures akisilikiza kwa makini elimu ya kupinga ukatili dhidi ya watoto kutoka kwa Kaimu kurugenzi wa Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga Alex Enock.

Kaimu mkurugenzi wa Shirika la Save The Children mkoani Shinyinga Alex Enock akiendelea kutoa elimu kwa wanafunzi.

Wanafunzi wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga ukatili kwa watoto.

Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akitoa elimu kwa wanafunzi hao na kuwataka wakawe mabalozi wazuri kwa wenzao katika kuhakikisha wanapaza sauti kwa kutoa taarifa juu ya matukio ya ukatili ili yapate kushughulikiwa kabla ya kuleta madhara na kuzima ndoto zao.

Wanafunzi wakisikiliza elimu ya kupinga ukatili .

Wanafunzi wakisikiliza kwa makini elimu ya kupinga ukatili dhidi ya watoto.

Wanafunzi wakinyoosha mikono juu kutoa ishara ya kupinga vita dhidi ya watoto "Stunt" ambayo ni kauli mbiu ya shirika la Save The Children katika kuadhimisha miaka 100.

Ishara ya kupinga vita dhidi ya watoto Stunt ikiendelea kuonyeshwa.

Ishara ya Stunt ikiendelea kuonyeshwa ili kupinga vita dhidi ya watoto.

Ishara ya Stunt ikiendelea kuonyeshwa na wanafunzi hao wa shule ya Little Treasures.

Awali wanafunzi wa shule ya Little Treasure wakiingia kwenye ofisi za Shirika la Save The Children Shinyanga Mjini.

Wanafunzi wa shule ya msingi binafsi Little Treasure wakipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Save The Children nje ya ofisi za Shirika hilo na kuonyesha ishara ya kupinga vita dhidi ya watoto (Stunt).

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527