MBUNGE AOMBA KURA KWA KUTUMIA TOVUTI YA VIDEO ZA NGONO


Joachim B. Olsen.
Mbunge mmoja nchini Denmark Joachim B. Olsen ameamua kuweka tangazo la kampeni yake ya kuchaguliwa tena kuwa Mbunge nchini humo kwenye tovuti ya video za ngono.


Mbunge huyo alipoulizwa kwanini amefanya hivyo, akasema ni lazima uwafuate wapiga kura kila sehemu walipo jambo ambalo liliwaacha watu wengi katika hali ya mshangao.

"Ndiyo, mimi ambaye nimeweka lile tangazo lakini hakuna kingine kinachoendelea zaidi ya kuwafuata wapiga kura wangu popote walipo najua wengine limewafurahisha na wengine litawaachia maswali, lakini ni namna tu ya utafutaji kura katika uchaguzi ujao", amesema Olsen.

Joachim B. Olsen, mwenye umri wa miaka 41 kitendo chake hicho kimeungwa mkono na baadhi ya wabunge wa chama cha Liberal Alliance, ambao wamedai kuwa aina hiyo ya utafutaji wa kura, itamsaidia kupigiwa kura kwa wingi katika uchaguzi wa Juni, 2019.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post