MAREKANI, CHINA ZAENDELEA KUKOMOANA


Marekani inatafakari kuongeza ushuru kwa bidhaa zaidi za China zitakazoingia nchini humo zenye thamani ya dola bilioni 300 zikiwemo za kompyuta hatua inayoongeza zaidi mzozo wa kibiashara unaotikisa masoko ya fedha na kuchochea hofu kuhusu ukuaji wa uchumi wa dunia.

Taarifa hii inafuatia tangazo la China hapo jana la kuongezeko ushuru kwa asilimia 25 katika bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani zenye thamani ya dola bilioni 60. 

Mwakilishi wa biashara wa Marekani ametangaza kwamba orodha hiyo mpya ya bidhaa 3,805 ni hatua ya kuelekea kutekelezwa kwa kitisho cha rais Donald Trump wa Marekani cha kuongeza kiwango kikubwa cha ushuru cha asilimia 25 kwa bidhaa zote za China zinazoingizwa Marekani. 

Bidhaa zinazoguswa kwenye orodha hiyo ni pamoja na kompyuta, misumeno, samaki aina ya tuna na vitunguu swaumu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527