KOREA KASKAZINI YARUSHA MAKOMBORA MENGINE LEO KWA MARA YA KWANZA

Korea Kaskazini imerusha makombora ya kwanza tangu 2017. Msururu wa makombora ya masafa mafupi yamerushwa Juammosi na kuangukia karibu na Bahari ya Japan.


Korea Kaskazini imerusha makombora kadhaa ya masafa mafupi kutoka pwani yake ya mashariki Jumamosi, limesema jeshi la Korea Kusini. 

Wachambuzi wanasema Korea Kaskazini inaongeza shinikizo dhidi ya Marekani kwa kushindikana kupatikana makubaliano ya maana katika kutano wa kilele wa Febuari, Hanoi.

Jeshi la Korea Kusini awali lilisema yaliyorushwa ni makombora lakini baadae likashidwa kutoa maelezo zaidi.

Iwapo itathibitishwa kuwa ni uzinduzi wa makombora ya masafa mafupi basi yatakuwa ni ya kwanza kurushwa na Korea Kaskazini tangu uzinduzi wake wa mwezi Novemba 2017. 

Baada ya uzinduzi huo, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba uwezo wake wa kinyuklia umekamilika, na ikakubali kuanzisha tena mazungumzo na Marekani pamoja na Korea Kusini.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sarah Sanders amesem: "Tunanazo taarifa kuhusu hatua za Korea Kaskazini za usiku huu. Tutaendelea kuzifuatilia."

Korea Kusini imesema makombora hayo yalirushwa kutoka mji wa Wonsan wa Korea Kaskazini milango ya saa tatu asubuhi leo saa za Korea. Korea Kusini imeeleza kwamba inafanya uchunguzi kuhusu makombora hayo, ikishirikiana na Marekani.

Waziri wa Ulinzi wa Japan amesema makobora hayo yameanguka karibu na pwani na nchi hiyo, na kwamba Japan haiko katika kitisho chochote cha usalama.

Ijumaa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini Kang Kyung-wha alisema Korea Kaskazini inalazimika kuonyesha "hatua za uhakika" za kusitisha shughuli zake za kinyuklia iwapo inataka kuondolewa vikwazo ilivyowekewa.

Mapema wiki hii, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui ameonya juu ya matokeo yasiyofurahisha iwapo Marekani haitobadilisha msimamo wake kuhusu vikwazo vya kiuchumi ilivyoiwekea nchi yake.

"Hatua hii inaonyesha wazi kwamba Korea Kaskazini imekasirishwa na msimamo wa Marekani wa kuishinikiza nchi hiyo kusimamisha mpango wake wa kinyuklia lakini bila ya kuikubalia kuiondolea vikwazi ilivyoiwekea," amesema Harry Kazianis wa gazeti la Marekani la masuala ya kimataifa la The National Interest.

Wachambuzi wanasema haijalishi ni makombora ya aina gani yaliyorushwa, ujumbe uliokusudiwa na Korea Kaskazini bila shaka  umeshaifikia Marekani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post