ATSOKO WAADHIMISHA MIAKA 7 TANGU KUANZISHWA KWAKE NCHINI TANZANIA


Meneja mkuu wa Atsoko Tanzania, Rehema Julius akizungumza kwenye hafla ya kusherekea miaka saba ya kuanzishwa kwa kapuni hiyo ya vipodozi hapa nchini iliyofanyika katika Duka lao Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjöberg akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Atsoko Tanzania wakati wa hafla ya kusherekea miaka 7 ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo hapa Tanzania iliyofanyika katika duka lao Mlimani City jijini Dar ee Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa Atsoko wakifuatilia yanayoendelea kujili kwenye hafla ya kusherekea miaka saba ya kuanzishwa kwa kapuni hiyo ya vipodozi hapa nchini iliyofanyika katika Duka lao Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja

BALOZI wa Sweden nchini Anders Sjoberg amesema kuwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Sweden utazidi kudumishwa na hiyo ni katika kushirikiana katika masuala ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 7 tangu kuanzishwa kwa kampuni ya Kiswedish Atsoko iliyoanza mwaka 2012 kwa duka moja lililopo Mikocheni hadi kufikia maduka 7 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa sasa ambayo yanapatikana Mikocheni, Slipway-Masaki, Mbezi Beach - Shoppers, Mlimani City, City Mall, Samora Avenue na Quality Centre Anders amesema kuwa wanasherekea miaka 7 ya Atsoko ikiwa na maendeleo lukuki na bado wanaendelea kuangalia njia zaidi za kutoa fursa kwa watanzania kupitia Atsoko.

Amesema kuwa nchini Tanzania soko ni zuri na kumekuwa na ushindani mkubwa hali inayowapa moyo katika kutoa fursa zaidi ili kujenga nchi ya viwanda na kuhusu kutoa ajira Balozi Anders amesema kuwa wamekuwa wakitoa vipaumbele kwa wanawake katika ajira na hiyo ni katika kuwainua zaidi katika suala zima la kiuchumi.

Amesema kuwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili utazidi kuimarika zaidi huku akihaidi kuendelea kushiriki katika kuendeleza shughuli za kijamii na kiuchumi.

Kwa upande wake Meneja mkuu wa Atsoko Tanzania Rehema Julias amesema kuwa, kusheherekea miaka 7 pia wamezindua bidhaa mpya ya Makeup inayoitwa Note. Ni bidhaa nzuri kutoka Uturuki ambayo inakidhi viwango vya kimataifa na imetengenezwa kwa ajili ya soko la Afrika.

Amesema kuwa kupitia Atsoko vijana na wanawake wamepata ajira na kujiajiri wenyewe huku akiwahakikishia watanzania ubora kwa bidhaa hizo kimatumizi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post