ATAKAYEKUTWA NA MFUKO WA PLASTIKI KUANZIA JUNI MOSI KULIPA FAINI 30,000


Ofisa Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Innocent Byarugaba 

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA 

HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha ,imeweka bayana kuwa kwa jamii kuwa,mtu yeyote atakaekutwa na mfuko wa plastiki kuanzia Juni mosi ,mwaka huu ,atatakiwa kulipa faini ya sh .30,000. 


Aidha halmashauri hiyo,imeendelea kutoa rai kwa wafanyabiashara na wananchi kuzingatia katazo la serikali la kutoendelea na matumizi ya mifuko hiyo ya plastiki kufungia bidhaa ifikapo siku hiyo. 

Ofisa Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Innocent Byarugaba ,akiongelea juu ya suala hilo kwa waandishi wa habari alieleza, katazo hili ni kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004, sura 191. 

Alisema, wafanyabishara, wanunuzi na wachuuzi wengine wametakiwa kutumia mifuko rafiki wa mazingira hasa inayotengenezwa na wajasiliamali wadogo ili kulinda mazingira na kuinua kipato chao. 

Katika hatua nyingine ,ofisa mawasiliano huyo anabainisha, halmashauri hiyo pia imeanza ujenzi wa machinjio ya kisasa eneo la Mtakuja itakayogharimu sh.bilioni 1.968.505.1. 

“Kampuni iliyochukua kandarasi hiyo ni PETRA ya jijini Dar-es-Salaam kwa gharama ya sh.bilioni 1,858,505,115. na gharama ya mtaalam mshauri milioni.120 ambaye ni AMUL ARCHITEC”,:”Fedha hizi ni ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mfuko wa uboreshaji na uendelezaji miji (ULGSP)”aliongezea kusema. 

Byarugaba alisema, lengo la halmashauri ya mji wa Kibaha ni kulinda afya za walaji kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanakula kitoweo 
kilichoandaliwa kwenye mazingira safi kiafya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post