ZIMBABWE YATOA TAHADHARI YA ATHARI ZA KIMBUNGA KENNETH...KWA SASA KIMESHATUA VISIWANI COMORO | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, April 25, 2019

ZIMBABWE YATOA TAHADHARI YA ATHARI ZA KIMBUNGA KENNETH...KWA SASA KIMESHATUA VISIWANI COMORO

  Malunde       Thursday, April 25, 2019
Taarifa ya wizara ya habari Zimbabwe imeeleza kwamba, Kimbunga Kenneth kinachotarajiwa kuzikumba nchi za Msumbiji, Malawi na baadhi ya maeneo ya Zimbabawe kimeingia visiwa vya Comoro.


Kimbunga hicho kimefika daraja la nne kikiambatana na upepo wa kasi ya 130 mph karibu na eneo la kati na kinaarifiwa kuelekea Msumbiji katika jimbo la Cabo Delgado.

Wataalamu wa hali ya hewa wanaonya kuwa kimbunga Kenneth kinatazamiwa kuwa na nguvu sawa na kimbunga Idai ambacho kilizikumba nchi tatu Msumbiji, Zimbabwe na Malawi mwezi uliopita na kusababisha maafa makubwa.

Taarifa kutoka Zimbabwe zinasema kwamba kutokana na uzoefu wa athari ya kimbunga Idai mwezi uliopita, watu wote wanaoishi katika maeneo hatarishi kama Mbire Muzarabani na maeneo ya chini ya jimbo la Masvingo na kwingineko wanatakiwa kujihadhari mapema.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post