UFARANSA YAKANUSHA MADAI YA KUMUUNGA MKONO MPINZANI WA SERIKALI YA LIBYA


Ufaransa imekanusha vikali madai ya Libya kuwa, inamuunga mkono Kamanda wa kijeshi Khalifa Haftar, anayeongoza vikosi vyake kujaribu kuliteka jiji kuu, Tripoli.

Waziri wa Mambo ya ndani wa Libya Fathi Bach Agha ametangaza kusitishwa kwa mahusiano kati ya serikali yake na ile ya Ufaransa kwa madai ya kuwaunga maadui wake.

Wakari uo huo, wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa wameanza majadiliano kuhusu  namna ya kuwezesha pande zote mbili kusitisha mapigano.

Wiki iliyopita, Kanali Mohamad Gnounou, msemaji wa vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa (GNA) alishtumu vikosi vya Jenerali Khalifa, kuweza kuingia sehemu ya mji na kupiga picha na baadae kuondoka na kurudi kwenye ngome zao.

Hata hivyo mapigano bado yanaendelea pembezoni mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli. Baadhi ya raia wa maeneo hayo wametoroka makaazi yao.

Shirika la msalaba mwekundu liimeripoti kuuawa kwa mamia ya watu na wengine kujeruhiwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post