Ajali imetokea leo Aprili 21, 2019 baada ya magari mawili ya mashindano kugongana eneo la Oldonyosambu, Arumeru jijini, Arusha na kuua na kujeruhi baadhi ya watu waliokuwa nje ya barabara.
Kati ya magari hayo mawili yaliyopata ajali, moja lilikuwa linaendeshwa na Mkenya na lingine Mtanzania.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shanna akiongea amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema atatoa taarifa kamili baada ya saa moja.