MWANAMKE AUAWA AKITAKA KUBAKWA

Regina Manday (35), aliyekuwa anafanya kazi kwenye shamba la mwekezaji Rift Wall Plantation Kijiji cha Magara Halmashauri ya Babati, ameuawa katika harakati za kubakwa.

Taarifa ya mama huyo kuuawa ilitolewa mwishoni mwa wiki na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Augustino Senga, na kusema tukio hilo lilitokea Aprili 15, mwaka huu saa 1:00 usiku, baada ya kupigwa mweleka na kuanguka chini.

Kamanda Senga alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo ni Claud Swedi maarufu kama Claud Safari (35), mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Moya, na amekamatwa.

“Chanzo cha mauaji haya marehemu alikuwa anakwenda kulala kambini kutokana na kufanyakazi za kibarua… wakati anapita maeneo ya korongoni kwenye mto, ndipo alipigwa mtama na kuangukia kisogo na kufariki dunia,” alisema Senga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post