MSIMU WA TATU WA “SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH” WAMALIZIKA, WASHINDI WAJIZOLEA ZAWADI



Meneja wa bidhaa wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Ester Raphael akizungumza na vyombo vya habari wakati wa fainali za mashindano ya ‘Smirnoff Ice Black Dj Search’ yaliyofanyika usiku wa Jumamosi katika viwanja vya Life Park-Mwenge.



Meneja wa bidhaa wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Ester Raphael akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa Msimu wa tatu wa shindano la ‘Smirnoff Ice Black Dj Search’ ‘DJ KG ambaye jina lake halisi ni Idrissa Kabika baada ya kuibuka mshindi wa fainali hizo, mshindi huyo alipewa Vifaa vya kazi (DJ kits) pamoja na Laptop.


Mtangazaji maarufu nchini, Hamisi Mandi maarufu kama B-Dozen akimpongeza mshindi wa shindano la ‘Sminorff Ice Black Dj Search’ ‘DJ KG ambaye jina lake halisi ni Idrissa Kabika’ baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza wa fainali hizo kwa mwaka 2019.

Mmoja wa washiriki wa shindano la ‘Smirnoff Ice Black Dj Search’ akionyesha ujuzi wake wakati wa fainali zilizofanyika Jumamosi jijini Dar es salaam.

Mmoja wa majaji wa Shindano la ‘Smirnoff Ice Black Dj Search’ Immanuel John maarufu kama ‘DJ Summer’ akizungumza wakati wa fainali za shindano hilo zilizofanyika Jumamosi, April 13 , 2019 jijini Dar es salaam.

***
Dar es Salaam. Aprili 14, 2019. Hatimaye msimu wa tatu wa wa shindano la ‘Smirnoff Ice Black Dj Search’ kwa mwaka 2019 umemalizika huku DJ KG akiibuka mshindi kwa kuwapiku maDj sita walioshiriki kwenye fainali hizo.

DJ KG ‘DJ KG ambaye jina lake halisi ni Idrissa Kabika kutoka Mkoa Dar es Salaam alitangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa shindano hilo ambapo jumla ya maDJ sita walishiriki na kudhaminiwa na kinywaji cha Smirnoff Ice Black kinachozalishwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).

Akizungumza wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbu wa Life Park Mwenge, Meneja wa bidhaa wa SBL Ester Raphael alisema lengo ni kuibua vipaji vipya kweye tasnia ya muziki kupitia fani ya uburudishaji ‘DJ’ sanjari na kutoa hamasa kwa wateja wa bidhaa zao.

“Tunaamini kwa kupitia shindano hili, SBL itatoa msisimko kwa wateja wake na muziki mzuri na nafasi ya kipekee kuonyesha uwezo wa MaDj wanaochipukia,” alisema

Shindano hilo limefanyika katika mikoa mitano ikiwamo Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Mwanza na Arusha ambapo waliweza kuwapata maDj sita waliotinga hatua ya fainali.

Alitaja zawadi zinazotolewa kwa washindi ikiwamo vifaa vya Dj “Dj Kit,Laptop pamoja na Conrollers kwa washindi watatu.

“Ushindani wa msimu huu ni mkubwa sana na tumeona Madj wakipamana kwa hali na mali na hamasa imekuwa kubwa sana kwao na kwa wateja wa kinywaji chetu cha Smirnoff Ice Black,” alisema.

Katika fainali hizo, DJ KG kutoka Mkoa wa Dar es Salaam aliibuka mshindi wa kwanza na kuibuka na DJ kits pamoja na Laptop (Mac). Mmoja wa Majaji, Immanuel John ‘DJ Summer Tz’ alisema walizingatia zaidi ujuzi wa DJ pamoja na muitiko kutoka kwa watu wanaowasikiliza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527