RC AAGIZA POLISI WAMTAFUTE MGANGA WA JADI ALIYETAJA WACHAWI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, March 8, 2019

RC AAGIZA POLISI WAMTAFUTE MGANGA WA JADI ALIYETAJA WACHAWI

  Malunde       Friday, March 8, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoani humo kumsaka na kumkamata mganga wa jadi ambaye inatajwa aliwaibua na kuwaadhiri wachawi katika bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga.

Akizungumza Mkoani Rukwa, Mkuu huyo wa Mkoa ameonya kuwa hataki yaliyotokea Njombe yatokee Rukwa, na kuongeza kuwa mganga huyo wa kienyeji analindwa na kiongozi wa chama cha kisiasa na hivyo kumtaka askari polisi kumtafuta.

“OCS na vyombo vyako vifanye upepelezi wa kina na ukamate yeyote yule ambae ametoka nje ya mkoa huu, nje ya Kilyamatundu anayefanya shughuli hizi, kamata weka ndani fanya mahojiano ya kina, na wengine nimeambiwa hapa ni viongozi wa vyama vya kisiasa, usijali huyu ni chama tawala, huyu ni nani, kama ukijua kwa uhakika kamata mhoji mpaka kieleweke, sisi hatutaki kuletewa Lambalamba hapa", amesema Wangabo

Mapema mwezi Februari Mkoani Njombe kulizuka kwa sakata la mauaji ya watoto Njombe na kupelekea kuanzishwa kwa operesheni maalum ya kuwasaka waganga wa kienyeji ambao wanatajwa kuhusika na imani za kishirikina.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post