MVUA ZATAWALA MAZIKO YA RUGE MUTAHABA

Maziko ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba yanayofanyika leo Jumatatu Machi 4, 2019 katika Kijiji cha Kiziru, Bukoba mkoani Kagera yametanguliwa na mvua.

Maziko hayo yanatanguliwa na shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Ruge zinaanza katika viwanja vya Gymkhana uliopo Bukoba mjini kisha ikifika saa 8:00 mchana, safari ya kwenda Kiziru itaanza.

Leo mvua imetawala tofauti na siku ya jana ambayo hakukuwa na dalili ya mvua.

Wakizungumza na Mwananchi Digital wakazi wa Bukoba wanasema, wakati huu ni msimu wa mvua za masika ambazo kwa kawaida huendelea hadi Mei.

Felician Bashaija anasema mvua hizo zinanyesha kuanzia mwishoni mwa Februari 2019 ila ilikuwa ndogo ikilinganisha na inayonyesha leo.

Naye Godfrey Rugaimkamu amesema: “Leo ni siku ya baraka kwa Ruge maana siyo kwa mvua hii ambayo inaambatana na radi, wakati tumezoea mvua kidogo."

Hata hivyo, kutokana na mkoa wa Kagera kuwa kwenye uoto wa Ikweta mvua zake kuambatana na radi ni jambo la kawaida.

Na Rhobi Chacha, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527