MWANAFUNZI AUAWA KWA KUSHAMBULIWA NA MAJAMBAZI

Mwanafunzi mwingine wa chuo kikuu cha Jomo Kenyatta ameshambuliwa na genge la majambazi na kuuawa alipokuwa akimsindikiza mpenzi wake kuelekea nyumbani. 

Kevin Shawn Mugenda na mpenzi wake walivamiwa wakiwa katika eneo la Highpoint katika barabara kuu ya Thika nchini Kenya Jumatatu Machi 4,2019. 

Kwa mujibu wa taarifa za Citizen Digital, Mugenda aliuawa baada ya kukata kuwapatia majambazi hao pesa alizokuwa nazo na simu yake.

Kisa hiki kinatoka mwezi mmoja tu baada ya mwanafunzi mwingine kutoka katika chuo hicho kuuawa na genge la majambazi eneo la Gachororo mtaani Juja.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Jomo Kenyatta wamelaumu usimamizi wa chuo hicho kwa kulegea katika kuimarisha usalama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post