Friday, March 1, 2019

CHADEMA YAFUNGUKA LOWASSA KUREJEA CCM..."YEYE NI MTU MZIMA ANAJUA ANACHOKIFANYA"

  Malunde       Friday, March 1, 2019

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania kimesema kuondoka kwa mwanachama wake, Edward Lowassa na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) hakutakuwa na madhara yoyote.


Hayo yamesemwa leo Ijumaa Machi 1, 2019 na Katibu Mkuu wa chama hicho kikuu cha upinzani Tanzania, Dk Vicent Mashinji alipozungumza na Mwananchi muda mfupi baada ya Lowassa ambaye ni waziri mkuu wa zamani kutangaza uamuzi huo. 

“Tunamtakia maisha mema huko aendapo yeye ni mtu mzima anajua anachokifanya,” amesema Dk Mashinji.

Alipoulizwa iwapo uamuzi wa Lowassa unaweza kukitetelesha chama hicho kikuu cha upinzani Dk Mashinji amejibu kwa kifupi “It will never happen (haiwezi kutokea)”.

Na  Tausi Mbowe, MwananchiUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post