AUAWA KWA KUCHOMWA KISU MKONONI WAKIDAIANA RABA NYEUSI KAHAMA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, March 10, 2019

AUAWA KWA KUCHOMWA KISU MKONONI WAKIDAIANA RABA NYEUSI KAHAMA

  Malunde       Sunday, March 10, 2019

Rashid Mustapha akivaa nguo baada ya kumchoma kisu mkononi Daniel Mtambala Gudugudu - Picha na William Bundala
Kijana aliyejulikana kwa jina la Daniel Mtambala Gudugudu (30 mkazi wa Nyihogo Mjini Kahama ameuawa kwa kuchomwa na kisu kwenye mkono wa kushoto na Rashid Mustapha (48) mkazi wa Nyihogo wilaya ya Kahama. 

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Machi 9,2019 majira ya saa 12 jioni eneo la Nyihogo Transfoma, kata ya Nyihogo Mjini Kahama. 

“Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliotokana na kudaiana viatu raba nyeusi, mbinu iliyotumika ni kumchoma kisu mkono wa kushoto na kusababisha damu nyingi kutoka”,ameeleza Kamanda Abwao. 

"Daniel alikuwa anadai arudishiwe viatu vyake,na katika ugomvi huo wakaanza kushambuliana ndipo aliyenyang'anywa viatu,akachomwa kisu na kusababisha kifo chake",ameeleza Kamanda Abwao.

Amesema tayari mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kiupelelezi kukamilika. 

Habari kutoka eneo la tukio zinasema watu hao walikuwa wamelewa na kwamba aliyeua mwenzake alikuwa ana mdai pesa zilizotokana na kuuziana nyama,katika kudaiana huko ndipo mtuhumiwa akachukua viatu vya marehemu, marehemu akahamaki baada ya viatu vyake kuchukuliwa ugomvi ukaanza akidai arudishiwe viatu vyake ndipo akaambulia kuchomwa kisu.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post