WANAFUNZI WAFUNIKWA NA KIFUSI BAADA YA KUDONDOKEWA NA GHOROFA

Watu  kadhaa ikiwemo wanafunzi wanahofiwa kufunikwa na kifusi baada ya jengo moja lililoko katika maeneo ya Ita Faji kwenye mji kibiashara wa Nigeria, Lagos kuanguka mchana wa leo tarehe 13 Machi 2019.

Msemaji wa Shirika la Usimamizi wa Masuala ya Dharula nchini Nigeria, Ibrahim Farinloye ameeleza kuwa, jengo hilo lilianguka majira ya saa asubuhi.

Taarifa za awali zianeleza kuwa, vikosi vya uokoaji viko eneo la tukio kwa ajili ya shughuli za uokoaji majeruhi. Hadi sasa ripoti kamili ya majeruhi katika tukio hilo haijawekwa wazi na mamlaka husika, ingawa taarifa zinaeleza kuwa, jengo hilo lilikuwa na wanafunzi takribani 100.

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, ghorofa hilo lilikuwa na shule pamoja na makazi ya watu. Shule ilikuwa katika ghorofa ya juu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527