ASKARI WANNE MATATANI KWA KUINGIZA BANGI NA SIMU GEREZANI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amemuagiza Kamishna wa Jeshi la Magereza kuwasimamisha kazi askari wanne wanaodaiwa kushirikiana na wafungwa kuingiza bidhaa zisizotakiwa katika Gereza la Ruanda.

Baadhi ya vitu vilivyobainika katika gereza hilo ni dawa za kulevya aina ya bangi pamoja na simu za mkononi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Machi 22, 2019 mkoani hapa Masauni amesema amebaini jambo hilo baada ya kufanya ziara ya siku moja katika gereza hilo.

“Jana nilitembelea Gereza la Ruanda na kugundua askari kukosa maadili kwa kuwa wamekuwa wakishirikiana na wafungwa kuingiza bidhaa haramu. Naagiza askari hawa wasimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi wa kina,” amesema Masauni.

Masauni amemtaka kamishna huyo kuunda kamati ya kuchunguza mtandao wa kuingiza bidhaa hizo.

“Nilikamata simu 10 na na dawa za kulevya aina ya bangi. Huu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu Rais (John Magufuli) ametoka kukemea vitendo hivyo lakini bado wanaendelea,” amesema Masauni.

“Vitu nilivyovibaini vyote niliwakabidhi polisi kufanya uchunguzi na bahati nzuri ripoti ya uchunguzi nimekabidhiwa muda huu.”
Na Ipyana Samson, Mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527