BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA, AKALIA KUTI KAVU


Rais Magufuli ameonesha kukerwa  na Balozi mpya wa Tanzania nchini Zambia ambaye  baada ya kuapishwa kuwa balozi, amekuwa akizunguka hapa nchini kwa kisingizio cha kuaga badala ya kwenda kuripoti kwenye kituo chake cha kazi alichopangiwa.


Rais ameyasema hayo leo Alhamisi March 27, 2019 wakati akimuapisha balozi mpya wa Cuba, Valentino Mlowola .


"Nakuomba Mlowola nimekuteua, uende Cuba, kuna Balozi wa Zambia nimemteua kila siku namuona anazunguka kwenye ofisi anaaga, mara kwa Waziri Mkuu, mara Makamu wa Rais, mara Zanzibar.


"Mwacheni aendelee kuaga, akimaliza kuaga, Ubalozi atakuwa hana."  Amesema Rais Magufuli


==>>Zaidi, msikilize hapo chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527