BENKI YA AZANIA YAWAHAKIKISHIA WATEJA WAKE UBORA WA HUDUMA BAADA YA KUINUNUA BANK M


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya hatua ya benki yake kuinunua Bank M.
Wanahabari wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe wakati akiwataarifu juu ya hatua ya Bank M kununuliwa na Benki ya Azania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe akijibu maswali ya wanahabari wakati akiwataarifu juu ya hatua ya Bank M kununuliwa na Benki ya Azania mapema leo jijini Dar es Salaam.
**
Dar-es-salaam, 20 Machi 2019: AZANIA BANK leo imewahakikishia wateja wake kuwa itaendelea kutoa huduma za ubora wa hali ya juu kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa kipindi kirefu sasa. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.

 Hii ni baada ya Benki kuu ya Tanzania (BoT) kutoa tamko kuhusiana na kukamilika rasmi kwa mchakato wa kuhamishia Mali na Madeni ya iliyokuwa Benki M na kuzihamishia benki ya Azania.

 "Tumeingia kwenye makubaliano na BoT ya kuinunua benki M ya Dar es Salaam hatua ambayo itapanua soko letu katika sekta ya kifedha hapa nchini Tanzania. Ununuzi huu wa benki M unatarajiwa kuongeza ufanisi kupitia michakato iliyoboreshwa, utamaduni na kuongeza soko", Itembe amesema.

 Mnamo Agosti 2018, BoT iliiweka benki M chini ya uangalizi maalum kutokana na beki hiyo kushindwa kutoa huduma za kifedha kwa mujibu wa sheria inayosimamia mabenki.

 Ununuzi huu umefanikiwa baada ya benki ya Azania kutuma maombi na andiko kwenda BoT juu ya nia yake ya kuinunua Benki M, baada ya hapo majadiliano marefu baina ya wanahisa na Benki Kuu yaliendelea kwa miezi kadhaa.

 Benki ya Azania kupitia kwa wanahisa wake wakubwa ambao ni PSSSF (51.95%), NSSF(27.99%), EADB(0.51%),Wanahisa wadogo (0.34%) pamoja na wanahisa wapya (National Health Insurance Fund(17.42%) na Workers Compensation Fund (1.79%)) hatimae kufikia muafaka wa upatikanaji wa mtaji na ukwasi wa uendeshaji wa benki baada ya kuichukua Benki M.

 Itembe amesema aina hii ya ununuzi wa benki inajulikana kama “sheria ya uchukuzi wa kiutendaji”

 “Tuliona ununuzi wa benki hii ni muhimu kwa utendaji za benki ya ABL. Ukamilisho wa uambatanisho wa benki hizi mbili unatar matarajio yao kupitia mtandao na matawi ya Benki ya Azania na matawi matatu amabayo awali yalikuwa wakimilikiwa na Benki M.’’ Amesema .

Uamuzi wa kupewa taasisi hiyo ulifanywa katika mkutano wa mwaka ulifanyika Desemba 21, 2018 ambapo wanahisa walikubaliana kuongezea mtaji Benki ya Azania na kukaribisha wanahisa wapya ambao nao pia walikubali kuongeza mtaji iliyofanya Azania kuwa imara na kuweza kuipata Benki M.

 Uchukuzi huu umeipeleka Azania mbali zaidi kuongeza idadi ya matawi kutoka 19 hadi 22 na kuongeza mtaji wake kutoka billion 64 za kitanzania mpaka billion 181 za kitanzania wakati jeduwali la mizani kuvuka trilioni kutoka awali ambapo ilikuwa nusu trilioni.

 “Baada ya kipindi hiki cha siku 45 tunatarajia kufungua milango kwa wateja wote wa Benki M ambao watahudumiwa katika tawi lolote la ABL watakalopendelea nchini Tanzania. Pia mchakato huu utapelekea kubadili mwonekano wa matawi ya benki M ya Kisutu, Pugu na Arusha ili yafanane na yale ya benki ya Azania” amesema Itembe. 

Kwa mujibu wa Itembe, hatua hii mpya inaifanya ABL kuwa (Tier One bank) kwa namna yoyote ile haitabadilisha muundo wa utendaji kazi wa benki badala yake utaunganisha mifumo hii miwili.

 “Kama sehemu ya uendeshaji, Benki ya Azania itaendelea na utekelezaji wa mikakati yake ya kisera ya miaka mitano (Five-Year strategic plan) ambayo itafanyiwa maboresho ili kuendana na huu Muunganiko wa Benki hizi mbili. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha wateja wa iliyokuwa Bank M wanaendelea kupata huduma zilizo bora zaidi”.

 Mkurugenzi wa ABL pia amebainisha kuwa ni mpango wa benki kuendelea kufanya kazi kwa kutengeneza timu moja ambapo wafanyakazi wa Azania na wale waliokuwa wa benki M watachanganywa katika maeneo mbalimbali ya kazi na kukuza utamaduni wa utendaji bora na utawala bora. 

Itembe pia amesema kazi itaanza mara moja kutokana na alichokiita muunganiko mzuri wa Benki zote mbili kuwa na mfumo wa tehama unaoendana kwa kiasi kikubwa. hivyo haitakuwa ngumu sana kuhamisha taarifa (data).

 Pia Benki ya Azania imesema itaendelea kufanya maboresho na kutumia teknolojia ya kisasa ili katika kuwahudumia wateja wakubwa na wadogo kwa ubora na ufanisi zaidi. 

#### 

ABL Financial Performance for the Year 2018 Azania Bank recorded a very impressive financial performance in terms of profitability and assets growth for the year 2018 as compared to year 2017.

 During the year 2018 profit before tax of Azania bank was TZS 8.2 billion which is 231% increase as compared to TZS 2.5 billion recorded in year 2017 mainly due to increased investments on loans and advance which translated in increase in interest income from TZS 41.9 billion in year 2017 to TZS 50.1 billion recorded in year 2018. 

In terms of balance sheet growth, total assets as at 31st December 2018 was TZS 504.0 billion showing an increase of 29% from TZS 390.0 billion recorded in year 2017. Loans and advances have grown by 57% to TZS 292.7 billion recorded in year 2018 from TZS 186.7 billion recorded in year 2017. Furthermore, there has been improvement in quality of loans which has led to decrease of non-performing loans to 6.2% from 12.3% recorded in year 2017. During the year 2018 Azania bank continued with its strategy of improving financial services delivery where it opened two new branches one being Morogoro branch in Morogoro Region and the other one named Sokoine Branch opened in the Capital City of Dodoma.

 Furthermore, Azania bank has implemented state of art core banking system in year 2018 with enhanced core banking applications as well as Digital experience which gives Azania bank competitive advantage in banking business as well as in its Digital Transformation Journey to serving both Retail and Corporate Segments.

 Notes for the Editor

 Azania Bank whose formal name is First Adili Bancorp Limited, and is commonly referred to as Azania Bank, is a commercial bank in Tanzania. 

The bank was established in 1995, as First Adili Bancorp, by Tanzanian citizens, together with national pension funds and International financial institutions, including the East African Development Bank, the Swedish International Development Agency and an American merchant bank, Gerald Metals Inc. Currently Azania Bank is owned by larger by the Pension Funds over 98% (PSSSF and NSSF, NHCF,WCF) and others are EADB as well as over 50 minority shareholders. It typically onboard both retail and corporate client

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527