JAMAA AMNYONGA SIMBA HADI KUFA


Kama kuliwahi kuwapo duniani mtu aliyekuwa na uwezo wa kupambana na simba kwa mikono yake hadi kumuua mtu huyo ni lazima awe ni Samsoni kwani maandiko ya Bibilia yanasema alikuwa mtu mwenye nguvu za ajabu.

 Lakini juzi kulitokea mtu mwingine anayeweza kulinganishwa na Samson katika eneo la kaskazini mwa Colorado, Marekani

Mwanamume huyo alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia na hakuwa na silaha yoyote na hivyo ilimbidi kujitetea kwa jiwe kisha mikono yake na akafaulu kumuua simba huyo.

 Kwa mujibu wa ripoti ni kwamba, maafisa wa sekta ya uhifadhi wa wanyama pori walisema mwanamume kutoka eneo la kaskazini mwa Colorado, Marekani alimuua simba kwa kumnyonga, baada ya mnyama huyo kumvamia ghafla. 

Inaelezwa kuwa mwanamume huyo alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia karibu na makavazi ya Fort Collins wakati alipovamiwa na simba huyo kutoka nyuma. 

Msemaji wa mbuga ya Colorado Rebecca Ferrell alisema kuwa mwanamume huyo alifahamisha maafisa wa uchunguzi kuwa alimnyonga simba huyo hadi kufa, jambo ambalo lilithibitishwa na ripoti ya upasuaji iliyofanyiwa mzoga wa simba huyo. 

Ferrell alisema kuwa mwanamume huyo alifanya vyema kwa kupigana na mnyama huyo kujitetea kadri ya uwezo wake. 

Kwa kuwa alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia, hakuwa na silaha yoyote na hivyo ilimbidi kujitetea kwa jiwe kisha mikono.

 Ripoti ya Fox News ya Jumamosi, Februari 9 ilisema, baada ya vita vikali na kumuua mnyama huyo hatari, bwana huyo alijipeleka hospitalini kwa kuwa alikuwa amejeruhiwa usoni, mikononi, miguuni na mgongoni. 

 Uvamizi wa simba dhidi ya binadamu katika milima huwa haushuhudiwi kirahisi, kwani tangu 1990 ni watu 16 pekee waliovamiwa na wanyama hao na watatu kati yao waliuawa. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post