MTU NA DADA YAKE WAFARIKI KWA KUPIGWA SHOTI YA UMEME WAKIANIKA NGUO


Watu wawili wa familia moja, Zulfa Chami na Zuhura Chami wamepoteza maisha, baada ya kupigwa shoti ya umeme na kamba ya kuanikia nguo katika eneo la Pasua, Manispaa ya Moshi.

Zulfa (24) na Zuhura (28) wamefikwa mauti hayo leo wakati wakianika nguo.

Habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio na baadae kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi, Hamisi Issah zinaeleza kuwa ndugu hao wa familia moja walifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa shoti ya umeme.

"Ni kweli ni mtu na dada yake wamefariki dunia leo kati ya saa 3:00 na 3:30 asubuhi katika eneo la Pasua Manispaa ya Moshi", amesema Kamanda Issah.

Chanzo - Nipashe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527