AJIFUNGUA BILA KUJUA KAMA ANA UJAUZITO..ALIKUWA ANAENDELEA NA HEDHI KAMA KAWAIDA

Msichana mwenye umri wa miaka 18, ambaye alizirahi kwa muda wa siku nne baada ya kuumwa kichwa ameshangazwa kujikuta amejifungua mtoto wa kike.

Ebony Stevenson,kutoka Oldham,hakuwa anajua kama ana ujauzito na alienda kulala kwa sababu alikuwa hajisikii vizuri.

Msichana huyo alipelekwa hospitali mara baada ya kuonekana amepitiwa usingizi kwa muda mrefu hivyo waliamua kumpeleka kupata huduma ya afya na kubainika kuwa ana ujauzito.

Mtoto wake alikuwa amejificha katika mfuko wa uzazi ambao ulikuwa umejificha, jambo ambalo huwa linatokea mara chache.

Kati miji miwili ya uzazi, mmoja ulikuwa unaendelea kumfanya dada huyo kuendelea kutoa hedhi huku mji mwingine ukiwa unakuza mtoto.

Mji huo wa mimba ulikuwa umekaa katika mgongo jambo ambalo lilisababisha ujauzito usionekane.

Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa michezo na yoga hakuwa amepata muonekano wa mimba, kuugua muda wa asubuhi au kukosa hedhi yake.

'Huu ni muujiza'

Msichana huyu ambaye amejifungua kwa mara ya kwanza ,amesema kila kilichotokea kwake kupata mtoto kinamshangaza.

"Nina hofu namna nitakavyoweza kumlea mtoto wangu ,maana sikumuona hata wakati anatoka tumboni kwangu au kuhisi kuwa alikuwa tumboni kwangu, ila nafikiri kuwa ni mtoto mzuri sana"

" Huu ni muujiza mkubwa sana kwangu."Ebony alieleza.

Ebony alifanyiwa upasuaji wa dharura ili ajifungue mtoto wake,saa tatu baada ya kushtuka kwa nguvu kutoka kwenye usingizi mzito.

Mama yake binti huyo Stevenson, mwenye umri wa miaka 39 alisema kuwa alipiga simu ya dharura baada ya mtoto wake kuanza kuumwa na kuanguka bafuni.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post