DK. MENGI AJITOSA MATIBABU YA RUGE

Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhavile, amesemaMwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, yuko tayari kuchangia matibabu ya Mkurugenzi wa Vipindi vya Uzalishaji Clouds Media, Ruge Mtahaba, ambaye yuko Afrika ya Kusini kwa matibabu ya kibingwa.


Mhavile alitoa ahadi hiyo jana katika mahojiano maalum na Kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Kituo cha Luninga ya Clouds cha jijini Dar es Salaam.Alisema tayari amempa taarifa Dk. Reginald Mengi kuhusu kuugua kwa Ruge na ameahidi kumsaidia pindi kamati maalum iliyoundwa kukusanya michango itakapokamilisha taratibu.“IPP media inaungana na familia na ndugu jamaa na marafiki, kumchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya Ruge ili asimame tena. IPP ipo tayari kumchangia Ruge baada ya kumati kutoa maelekezo ya nini kifanyike," Mhavile alisema.Alisema taarifa za kuugua kwa Ruge alizipata mwaka jana akiwa India na alipomwona, alimpa pole na anaamini Ruge atapona na kuendelea na majukumu ya kujenga taifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post