ALIKIBA ATUHUMIWA KWA WIZI WA KAZI ZA WASANII...DOMOKAYA AMCHANA



Alikiba.
Msanii mkonge wa muziki wa Bongo Fleva, Domo Kaya amesema kuwa wasanii wapya kwenye muziki huo wanatakiwa kuwa wabunifu, baada ya msanii Alikiba kutumia kidokezo 'Yebaba' ambacho alikuwa alikitumia yeye mwanzo.

Domo Kaya amefunguka hayo kupitia FRIDAY NIGHT LIVE ya EATV, ambapo amesema kuwa Alikiba kutumia neno hilo sio vibaya lakini alitakiwa kuomba ruhusa kwanza kwake.

"Nawasihi wadogo zetu kuwa wabunifu, na kuacha ujanja ujanja maana kutumia kitu hukatazwi lakini uombe kwa muhusika akupe baraka zake", amesema Domo Kaya.
Msanii Domo Kaya.

Hivi karibuni msanii Alikiba ameonesha kutumia msemo huo 'yebaba' katika wimbo wake mpya wa 'Kadogo' aliouachia mwishoni mwa mwaka uliopita na kuupa umaarufu mkubwa kwa mashabiki wake badala ya ule ambao ulizoeleka wa 'Yooo', ambao alikuwa akiutumia hapo kabla.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527