UMOJA WA AFRIKA NA MAREKANI WALAANI SHAMBULIZI LA NAIROBI

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amelaani vikali shambulio la Hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi.


Katika taarifa yake, Faki amevisifu vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa kuchukua hatua za uokozi wa raia na kupambana na wahalifu mapema iwezekanavyo. Pia amesema tukio hilo linaonesha umuhimu wa kupitia upya mipango ya kuongeza nguvu ya kupambana na vikundi vya kigaidi barani Afrika.

Mwenyekiti wa Kamisheni anathibitisha utayari wa AU kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na Nchi Wanachama katika kupambana na visa vya ugaidi pamoja na harakati za kutuliza hali nchini Somalia na mapambano dhidi ya kundi al-Shabaab kupitia vikosi vyake vya AMISOM.

Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake nchini Kenya Bw Robert Godec ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Marekani inashutumu vikali shambulio hilo.


Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa raia wake mmoja ni kati ya watu waliopoteza maisha kwenya mkasa huo.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527