Tanzia : ALIYEZAWADIWA MILIONI 100 NA JPM KWA KUGUNDUA MADINI YA TANZANITE AFARIKI DUNIA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, January 30, 2019

Tanzia : ALIYEZAWADIWA MILIONI 100 NA JPM KWA KUGUNDUA MADINI YA TANZANITE AFARIKI DUNIA

  Malunde       Wednesday, January 30, 2019

 
Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, Jummane Ngoma enzi za uhai wake

Aprili 6 ,2018, Rais John Magufuli akiwa na mzee Jumanne Ngoma wakati akizindua ukuta wa mgodi wa Tanzanite, Mirerani mkoani Manyara ambapo Rais Magufuli alimzawadia Sh100 milioni kama shukrani kwa mchango wake kwa kugundua madini ya Tanzanite.

Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, Jummane Ngoma amefariki dunia leo Jumatano Januari 30, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mtoto wa marehemu, Hassan Ngoma,akizungumza na Mwananchi  amesema, “Ni kweli Mzee amefariki leo jioni hii hapa Muhimbili,” amesema Ngoma.

Hassan amesema kinachofanyika kwa sasa ni kuuhifadhi mwili wa baba yake kisha baadaye watatoa taarifa rasmi ikiwamo utaratibu wa msiba utakuwa wapi na mazishi yatafanyika wapi baada ya kikao cha familia.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post