SPIKA NDUGAI AMHAKIKISHIA RAIS MAGUFULI KUWA BUNGE SI DHAIFU

 

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa Bunge lake si dhaifu kama alivyosema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu na Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) iliyofanyika katika ofisi za Mamlaka ya Udhibiti wan Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo baada ya kuombwa na Rais Magufuli, Spika Ndugai amesema utekelezaji wa mradi huo ulitegemea sana maoni ya wabunge kabla ya kupitisha fedha hivyo ni ishara kuwa Bunge si dhaifu kwa sababu wamefanikisha suala hilo.

“Wakati bajeti hiyo inapitishwa kulikuwa na mjadala mkali kwa sababu wabunge walikuwa wanahitaji kujua kwa nini kodi inayotokana na matumzi ya simu ni ndogo kuliko idadi ya watumiaji wa simu.”

“Ilibidi tutengeneze sheria, hatukufaulu lakini ulipoingia madarakani ukasema jambo hili lirudishwe bungeni lifanyiwe kazi, ukasaini na hiki ndicho kilichotokea,” amesema Spika Ndugai

Amesema jambo hilo si dogo kwa wasiolewa na badala yake watu wanapenda giza hivyo mtambo huo ni tochi utakaoweza kumulika kuangalia sehemu ambayo haionekani vizuri na wasiopenda mwanga ni watu wenye pesa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527