RONALDO AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKWEPA KULIPA KODI

Nyota wa soka Cristiano Ronaldo amewasili mjini Madrid huku akiandamwa na idadi kuwa ya waandishi habari ambapo anakabiliwa na mashtaka ya kukwepa kulipa kodi ambayo huenda yakasababisha kupigwa faini ya €18.8m (£16.6m) .

Jaji mmoja alikataa ombi la mchezaji huyo kuhudhuria kesi hiyo kupitia kanda ya video ama hata kuingia katika jumba hilo kwa kutumia gari ili kuzuia kuandamwa na vyombo vya habari.

Anatarajiwa kukiri mashtaka hayo katika makubaliano ambayo yatamlazimisha kuhudumia kifungo cha mezi 23 jela.

Nchini Uhispania, wafungwa huwa hawahudumii kifungo cha chini ya miaka miwili.

Hali ya makosa ya Ronaldo inamaanisha kwamba hatohudumia kifungo jela.

Mchezaji huyo wa Juventus ambaye aliichezea klabu hiyo usiku wa kuamkia mashtaka hayo aliwasili akiwa anatabasamu.

Wakili wake alikuwa amehoji kwamba kutokana na umaarufu wake , alipaswa kutotumia lango kuu la mahakama kutokana na hali ya usalama.

Así ha llegado Cristiano Ronaldo a la Audiencia Provincial. De la mano de Georgina, firmando autógrafos y sonriente: “Estoy perfecto”


Ronaldo ambaye ni bingwa mara tano wa taji la Ballon d'Or na kuwa miongoni mwa wachezaji bora duniani, anatuhumiwa kwa kukwepa kulipa kodi nchini Uhispania kati ya 2011 na 2014 wakati alipokuwa akiichezea klabu ya Real Madrid wakati huo akiwa na makao yake nchini Uhispania.

Kesi hiyo inaangazia mikataba ya haki za picha zake.

Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa fedha hizo zilipitishwa kupitia kampuni zinazotozwa kodi ya chini katika mataifa ya kigeni ili kukwepa kulipa kodi iliohitajika.

Kitita hicho kilidaiwa kuwa cha €14.8m.

Mwaka 2017, wakati madai hayo yalipochipuka, viongozi wa mashtaka walisema kuwa ulikuwa ukiukaji wa ahadi yake nchini Uhispania.

Lakini wakili wa Ronaldo alisema kuwa kutoelewana kuhusu kile kilichohitajika na kili ambacho hakikuhitajika chini ya sheria za Uhispania na kuzuia jaribio lolote la kukwepa kulipa kodi.
Makubaliano hayo yaliofanyika mwezi Juni mwaka uliopita yaliafikiwa na mamlaka ya ushuru nchini Uhispania.

Yatawasilishwa mbele ya jaji siku ya Jumanne mahakamani.

Jaji huyo atatangaza uamuzi wake katika kipindi cha siku zijazo.

Ronaldo sio mchezaji wa kiwango cha juu wa pekee kukabiliana na mkono wa mamlaka ya ushuru nchini Uhispania.

Mchezaji mwezake wa zamani Xabi Alonso pia anatarajiwa kuwasili mahakamani siku hiyohiyo kwa mara ya kwanza akishtakiwa na shataka kama lake la makosa ya haki za picha zake ya takriban €2m.

Ronaldo pia anakabiliwa na shtaka jingine: Mchezaji huyo anatuhumiwa kutekeleza ubakaji mjini Las Vegas 2009, mashtaka ambayo anapinga.
Chanzo : Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527