RAIS MAGUFULI: CHANGAMOTO ZILIZOPO SASA ZISIPOTATULIWA, SIDHANI KAMA AJAYE ATAZITATUARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema hana uhakika endapo mrithi wake ataweza kutekeleza mambo anayoyafanya katika uongozi huu wa awamu ya tano.

Magufuli ameyasema hayo jana Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Alisema katika safari ya kutatua changamoto anakutana na magumu mengi na ndiyo maana amekuwa akihitaji nguvu za Mungu kutekeleza majukumu yake.

“Viongozi wa dini endeleeni kuliweka Taifa hili kwenye mikono ya Mungu. Hii ni vita kama ilivyo nyingine na vita ya uchumi inahitaji maombi sana, bila maombi kazi hii haiwezi kufanyika,” alisema.

“Hao wanaokaa gizani hauwezi kujua ana kisu, ana panga au ameweka nyoka mfukoni lakini huko gizani huwa wanatolewa kwa maombi, yatawapumbaza huko gizani wasitake kufanya walichokusudia.”

Alisema kufanya hivyo kutawafanya viongozi wa nchi kusimamia misingi ya uadilifu na upendo wa kweli katika kulitumikia Taifa tajiri, lenye changamoto nyingi zinazohitaji kutatuliwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post