MANNY PACQUIAO AVAMIWA NA WATU WASIOJULIKANA LOS ANGELES

Nyumbani kwa Manny Pacquiao Los Angeles mjini Los Angeles.

Nyumba yake ambayo ipo Los Angeles Marekani ilivamiwa muda mchache tu baada yakushinda pambano lake dhidi ya Adrien Broner.

Ripoti iliyotolewa na Polisi wa mjini Los Angeles imeeleza kuwa nyumba hiyo ilivamiwa usiku wa Jumapili na wezi ambao hawakuweza kuiba chochote kutokana na wana usalama hao kuwahi eneo la tukio na kudhibiti hali hiyo.

Polisi wameeleza kuwa walitumiwa ujumbe juu ya kuwepo kwa wezi hao na mtu mmoja katika timu ya Pacquiao hivyo wakawahi kwa polisi.

Pacquiao alishinda pambano hilo dhidi ya Adrien kwa pointi na baada ya pambano hilo la (WBA world welterweight) akaweka wazi kuwa anahitaji kurudiana na bondia Floyd Mayweather ambaye alimpiga mwaka 2015.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527