MO SALAH ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA

Mohamed Salah alikabidhiwa tuzo hiyo na rais wa Caf Ahmad Ahmad (kushoto) na rais wa Liberia George Weah (kulia)


Mshambuliaji wa Misri na klabu ya Liverpool ya England Mohamed Salah ndiye Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Soka Barani Afrika kwa mwaka 2018 - hii ikiwa ni mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo.

Salah, 26, alimshinda mwenzake wa Liverpool Sadio Mane kutoka Senegal na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.

Alikabidhiwa tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika nchini Senegal Jumanne januari 8,2019.

"Nimekuwa na ndoto ya kushinda tuzo hii tangu nilipokuwa mdogo na sasa nimefanya hivyo mara mbili mtawalia," Salah alisema.

Salah amefunga mabao 16 katika mechi 29 alizoichezea Liverpool mashindano yote msimu huu.

Salah, Mane na Aubameyang wamo kwenye Kikosi Bora cha Mwaka Afrika pamoja na beki wa Manchester United Eric Bailly, kiungo wa kati wa Manchester City Riyad Mahrez, kiungo wa kati wa Liverpool Naby Keita na beki wa kushoto wa Tottenham Serge Aurier.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527