KIGWANGALLA,FATMA KARUME WATISHANA KWENYE MNUSO



Fatma Karume kushoto na Hamis Kigwangalla kulia.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla mchana huu anakutana na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, huku kila mmoja akitamba kuwa atashinda kwenye mkutano huo

Viongozi hao wawili wanakutana katika mzungumzo ambayo yanahusisha chakula cha katikati ya asubuhi na mchana maarufu kama 'Brunch' ambayo wao wameamua kuiita 'Brunch date' huku kila mmoja akitamba ataibuka mshindi kwa kula pamoja na hoja.

Mapema leo Fatma ameanzia kwenye mazoezi huku akimtahadharisha Kigwangalla kuwa mazoezi hayo ni kwaajili yake hivyo ajipange na 'Wallet' yake vinginevyo atakosa pesa ya kulipia na ataosha vyombo'

Wallahi @HKigwangalla I am not going DUTCH for this BRUNCH. I mean it so you really had better come with your WALLET. Maana nitakuacha pale Hyatt usafishe vyombo mimi nitasepa ! 🤣🤣🤣

65 people are talking about this
Naye Kigwangalla amejibu kwa kumtishia Shangazi kuwa atamshinda na endapo atamletea uzungu mwingi kwasababu ni mtoto wa kishua na yeye ni mtoto wa uswahilini atatumia lugha ya Kinyamwezi kummaliza.

Ndiyo nimetoka mazoezini sasa hivi, nimearifiwa shangazi anajipanga! Haya bhana, tutaona leo nani Konki zaidi! 💪🏾

60 people are talking about this


'Brunch date' yao hiyo ilianza kwa mabishano ya hoja katika mtandao wa Twitter kabla ya kukubaliana wakutane kushindanisha hoja hizo katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam ndipo Shangazi akamwambia ahakikishe na msosi wa kutosha unakuwepo.

Wawili hao wakiwa njiani kuelekea eneo la tukio.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527