Fatma Karume na Waziri Kigwangalla
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Fatma Karume wamekutana leo kwenye 'Brunch date' na kujadili jinsi ya kuboresha uhusiano baina ya viongozi wanaowasiliana kwa kutumia mitandao.
Baada ya mkutano huo ambao umedumu kwa zaidi ya masaa kadhaa ukianza majira ya saa 7:00 mchana hadi saa 12:00 jioni, umemalizika kwa wawili hao kuonekana wakifurahia na kuonesha umoja tofauti na jinsi ambavyo huwa wanacharuana mitandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Waziri Kigwangalla amesema mambo yote yamewekwa kando huku akisifu kuwa Fatma maarufu Shangazi ni mtulivu na msikivu sana.