Friday, January 25, 2019

MATOKEO YA MTIHANI SHULE YA 'MASELA' GUMZO...WAMEACHA MSELA WAO MMOJA

  Malunde       Friday, January 25, 2019

 
Baada ya Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) kutangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, kuna mambo mengi ya kushangaza na kufurahisha kuhusu matokeo hayo yaliyoibua mjadala mitandaoni.

Mathalan, shule ya sekondari Tumaini iliyopo Morogoro kutumia polisi kufanya udanganyifu.

Wahusika katika shule hiyo walivunja ukuta wa chumba cha kufanyia mtihani na kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha pili ambao siku ya mtihani walikuwa wakipewa mitihani na kuwapeleka walimu.

Sasa achana na hiyo ya sekondari ya Tumaini, kuna hii ya Shule ya Sekondari Masela.

Baada ya matokeo hayo kutangazwa wapo waliofananisha maana ya neno ‘masela’ wanavyolitumia mtaani, na matokeo ya shule hiyo.

Msela ni mtu ambaye haoni matatizo, yaani hufanya anachotaka na hajali watu watafikiri nini.

Kwa matokeo ya shule hiyo wapo waliofananisha na maana ya neno msela ingawa kiuhalisia jina la shule hiyo halina maana ambayo watu wanadhani.

Shule hiyo ina watahiniwa 15, kati yao ni mmoja tu ndio amepata daraja sifuri.

Watahiniwa wawili walipata daraja la pili, waliopata daraja la tatu wawili na waliopata daraja la nne wanane.

“Masela wamemuacha msela wao mmoja tu, yaani wao wamefaulu ila msela wao mmoja kabaki (akimaanisha aliyepata daraja sifuri),” amesema mmoja wa wafuatiliaji wa matokeo hayo mtandaoni.


Kuwa Mjanja..Download App mpya ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako


  Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
  Loading...
  logoblog

  Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

  Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
  https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
  Previous
  « Prev Post