MAGAIDI WALIOSHAMBULIA NAIROBI WAUAWA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema  oparesheni ya kukabiliana na washukiwa wa ugaidi waliovamia hoteli ya Dusit2 mjini Nairobi imekamilika na kwamba washambuliaji wote wameangamizwa.

Watu waliyokuwa wamejihami kwa silaha siku ya Jumanne walivamia jengo la hoteli ya kifahari ya Dusir2 katika eneo la Westlands katika jiji kuu la Nairobi nchini Kenya na kuwaua watu 14.

Awali maafisa walitangaza kuwa oparesheni hiyo ilikamilika saa kadhaa baada ya shambulio hilo lakini mlilio ya risasi na milipuko ilisikika mapema alfajiri ya leo (Jumatano)


Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab, limedai kuhusika na shambulio.

Haijabainika ni washambuliaji wangapi walihusika na shambulio hilo.

Akihutubia taifa kwa moja kwa moja kupitia televisheni kutoka Ikulu, rais Kenyatta amesema kuwa watu 14 waliuawa katika shambulio hilo na wengine 700 kuokolewa kutoka jengo hilo.

Shirika la msalaba mwekundu hata hivyo limeripoti kuwa waliyofariki katika mkasa huo ni watu 24.

Raia wa Marekani ni miongoni mwa waliyofariki, imesema wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Raia mmoja wa Uingereza pia anahofiwa kufariki dunia.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527