YANGA WAMJIBU MANARA SAKATA LA KULIPA KODI TRA

Klabu ya soka ya Yanga imetoa jibu kwa msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, aliyehoji juu ya utaratibu wa kuchangisha fedha kwa wanachama wake kama ni halali na unakatwa malipo ya kodi kwa serikali.


Kupitia ripoti yake ya michango ya fedha za mashabiki kwa miezi miwili ya Novemba na Desemba Yanga imeweka wazi kuingiza kiasi cha shilingi 5,165,009 kwa mwezi Desemba na 563,737 kwa mwezi Novemba.

Katika ripoti hiyo Yanga imeeleza michango hiyo imefanyika kwa njia ya simu kupitia Selcom Wallet hivyo lazima kodi zote sitahiki zitakuwa zimelipwa.


Manara alihoji juu ya suala hilo hivi karibuni baada ya kusambaa video mtandaoni ikiwaonesha wachezaji wa Yanga wakipewa fedha na mashabiki baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City uliopigwa jijini Mbeya.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post