Picha : BASI LA FIKOSHI LAPINDUKA NA KUUA WATU WANNE, KUJERUHI 42

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 42 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya FIKOSHI lenye namba za usajili  AUV 400 linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Mwanza kupoteza mwelekeo na kupinduka katika eneo la Mnarani wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi aliokuwa nao dereva wa basi hilo, na kusababisha kupinduka.

“Ajali imetokea maeneo ya Uvinza, kuna sehemu inaitwa Mnarani, ni barabara ya Vumbi, ilipofika maeno hayo ambayo ina kona kona nyingi, kwa mujibu wa mashuhuda wamesema dereva alikuwa kwenye mwendo kasi, alipofika maeno hayo, gari ikapinduka na kusababisha vifo vyo watu wanne wanaume watatu na mwanamke mmoja, na majeruhi 42.

"Majeruhi tumewachukua kuwapeleka hospitali ya Maweni ya Mkoa ambako wanaendelea kupata matibabu”, amesema Kamanda Otieno.

Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog 

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527