Ofisa elimu maalum wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu,mkoani Arusha Martin Goi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Tukio hilo lililothibitishwa na mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo limetokea juzi jioni Jumatatu Januari 14, 2019 katika mgahawa wa Rhotia Garden mjini Karatu.
Goi alipigwa risasi mbili kifuani na kukimbizwa Hospitali ya Selian mjini Arusha kwa matibabu na kufariki dunia jana Jumanne Januari 15, 2019.
Na Mussa Juma, Mwananchi