ZITTO NA WENZAKE WAULILIA UHURU

Leo, Desemba 9 ni siku ya kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) ambao ulipatikana mnamo mwaka 1961 chini ya uongozi wa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Katika kuikumbuka siku hii muhimu, Kiongozi wa Chama cha ACT-wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ametumia kupaza sauti juu ya hali ya demokrasia ya vyama vya siasa ilivyo nchini hasa katika Muswada wa Mabadiliko ya Sheria za Vyama Vya Siasa uliopendekezwa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Zitto Kabwe ameandika, "1961 tulipata Uhuru na kujitawala. 1965 tukawa nchi ya Chama kimoja cha Siasa. 1992 tukagundua makosa na kurejea kwenye siasa ya vyama vingi vya siasa. 2018 umependekezwa muswada wa vyama vya siasa ili ifikapo 2019 turudi kwenye ‘defacto’ Chama Kimoja Cha Siasa".

Pia katika kupinga muswada huo, Zitto amesema kuwa chama chake cha ACT pamoja na vyama vingine 14 vimeazimia kufanya mkutano wa pamoja na wanahabari leo jijini Dar es salaam ili kutoa tamko la pamoja kuhusu Mswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527