RAIS MAGUFULI ATANGAZA KUSAMEHE WAFUNGWA 4,477

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Dkt. John Magufuli ametoa salamu za Kumbukumbu ya Miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara, leo Ijumaa, Desemba 7, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akituma salam hizo, Rais Magufuli kwa mujibu wa Ibara ya 45 Ibara ndogo ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametangaza msamaha kwa wafungwa 4,477 waliokuwa wamefungwa / kuhukumiwa kwenye magereza mbalimbali nchini ambapo kati yao 1,176 wataachiwa Desemba 9, 2018 katika Sikukuu ya Uhuru.


“Wafungwa 1,076 watatoka siku ya Maadhimisho ya Uhuru yani December 9, 2018, msamaha huu utawahusu Wafungwa Wagonjwa, Wazee kuanzia miaka sabini na zaidi, Wafungwa wakike walioingia Gerezani wakiwa Wajawazito” 

“Nimeamua Wafungwa waliotumikia robo ya adhabu zao wapunguziwe robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la theluthi moja” -Rais Magufuli

“Msamaha hautawahusu Wafungwa wanaotumikia baadhi ya adhabu zikiwemo Kunyongwa, Kifungo cha maisha, biashara ya Dawa za kulevya, biashara za Binadamu, kukutwa na viungo vya Binadamu, Walionajisi, Waliowapa mimba Wanafunzi” -Rais Magufuli

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527