ALIYEBEBA MBUZI KWENYE TAIRI LA NYUMA ACHUKULIWA HATUA


Benki ya TIB imetoa taarifa ya kusikitishwa kwake na kitendo cha dereva wa gari inayomilikiwa na benki hiyo yenye namba za usajili SU 38431 cha kubeba mbuzi kwenye tairi ya akiba iliyopo nyuma ya gari.

Kwenye taarifa hiyo ambayo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Tawi la Mlimani City, imeeleza ni kwa namna gani dereva huyo ametumia mali ya umma vibaya, na pia kukiuka haki za wanyama.

Benki hiyo imesema itamchukulia hatua stahiki dereva huyo, ambaye alikuwa akiendesha gari hilo kutoka Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post